Corona yaua 10 zaidi, 1,048 wakikutwa na virusi hivyo

0

Maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona nchini yameongezeka na kufikia 1,349 baada ya wagonjwa 19 zaidi kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amearifu kuwa watu wengine 1,048 wamekutwa na virusi hivyo katika muda huo wa siku moja baada ya kupima sampuli 8,660 na kufikisha idadi ya visa hivyo kuwa 75,193.

Idadi ya waliopona ugonjwa huo imeongezeka na kufikia 50,984 baada ya watu wengine 326 kupona, 107 walikuwa hospitalini huku wengine 219 wakipona wakiwa nyumbani.

Kwa sasa, wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali kwa kuugua ugonjwa huo 1,114 huku wanaoshughulikiwa nyumbani wakiwa 6,332.

Waziri Kagwe vile vile ameripoti kuwa wagonjwa waliolazwa katika chumba cha watu mahututi ICU ni 52 huku wanaosaidiwa na mashine kupumua wakiwa ni 28.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here