Corona yamuua aliyekuwa waziri Joe Nyaga

0

Aliyekuwa waziri mwenye ushawishi mkubwa Joe Nyaga ameaga dunia.

Familia yake imesema Nyaga mwenye umri wa miaka 72 amefariki kutokana na matatizo yanayoambatana na corona katika Hospitali ya Nairobi.

Nyaga aliyezaliwa mwaka 1948 alikuwa waziri wakati wa uongozi wa rais Daniel Moi kabla ya kuhudumu kwenye baraza la mawaziri wakati wa serikali ya muungano iliyoongozwa na rais mstaafu Mwai Kibaki na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.

Nyaga aliyekuwa waziri wa vyama vya ushirika na mwanachama wa vuguvugu la ‘Pentagon’ aliwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2017 kama muwaniaji huru lakini akashindwa.

Nyagah vile vile alihudumu kama balozi wa Kenya mjini Brussels na Ubelgijimiaka ya themanini na pia alihudumu kama mbunge wa Gachoka mwaka 1998.

Mwaka 2013, hakuwania wadhifa wowote kisiasa na alikuwa anapigiwa upato na wengi kuchukua uongozi wa kisiasa kutoka kwa rais Uhuru Kenyatta mwaka 2022.

Babake Jeremiah Nyagah alikuwa waziri wakati wa utawala wa rais Moi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here