Chief Kariuki afariki dunia

0

Chifu maarufu kutoka eneo la Lanet Umoja katika kaunti ya Nakuru Francis Kariuki ameaga dunia.

Familia yake imedhibitisha kwamba chief Kariuki anayefahamika na wengi kwa kutumia mtandao wa Twitter kuwataarifu kinachoendelea amefariki akipokea matibabu katika hospitali ya Nakuru Level Five.

Marehemu alitambuliwa duniani kote kutokana na juhudi zake kuwafahamisha wenyeji wa eneo lake na ulimwengu kwa ujumla kuhusu yanayojiri.

Chief Kariuki tangu mwaka 2011 alitumia ukurasa wake wa Twitter kuripoti kuhusu kupotea kwa mifugo pamoja na visa vya ukosefu wa usalama katika eneo lake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here