Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imelitahadharisha taifa dhidi ya kiuvunjilia mbali tume hiyo kupitia mchakato wa BBI kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.
Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema mazoea ya kubadilisha tume ya uchaguzi kila baada ya uchaguzi imesababisha asasi hiyo muhimu katika usimamizi wa uchaguzi kukosa kuwa na udhabiti.
Chebukati amelalama kuwa muingilio wa tume hiyo na wanasiasa umehujumu uhuru wake na kuifanya kukosa uwezo wa kufanya maamuzi yake kama inavyotakiwa.
Mwenyekiti huyo vile vile amekosoa pendekezo la BBI kwamba makamishna wa IEBC wateuliwe na vyama vya kisiasa akisema watakosa kuwajibikia majukumu kwa mujibu wa katiba na badala yake wataegemea upande mmoja.