CHAMA CHA TND CHAKANA KUNUNULIWA NA GACHAGUA

0
NAIBU WA RAIS RIGATHI GACHAGUA AKIIHUTUBIA HADHARA
NAIBU WA RAIS RIGATHI GACHAGUA AKIIHUTUBIA HADHARA

Kiongozi wa chama cha The New Democrats Thuo Mathenge amesema kuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua hajachukua uongozi wa chama hicho kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari.

Thuo Amesema kuwa uongozi wa chama hicho haujabadilishwa ila kiko wazi kwa kila mtu kujiunga nacho ikiwemo Naibu Rais Gachagua.

Amedai kuwa chama hicho ndicho maarufu zaidi katika Mlima Kenya, akibainisha kuwa kitaleta mapinduzi katika siasa za eneo hilo mwaka wa 2027.

“Naibu wa Rais hajachukua uongozi wa chama hiki inavyoadaiwa ila tuko radhi kumpokea iwapo atataka kujiunga nasi. Tutakuwa na usemi mkubwa katika kuunganisha GEMA mwaka wa 2027” Amedai Thuo

Thuo aidha amedhibitisha kuwa Jimmy Kibaki; Mwanawe hayati Rais mstaafu Mwai Kibaki tayari amejiuzulu kama Naibu Mkuu wa Chama hicho na wanapanga kuandaa uchaguzi kusaka mridhi wake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Jimmy alisema anakihama chama cha The New Democrats “baada ya kufikiria na kutafakari sana kuhusu uamuzi huo.”

Thuo amebainisha kuwa chama hicho kwa sasa kinajishughulisha na harakati za usajili wa wanachama kote Nchini akidokeza kuwa watu mashuhuri wameonyesha nia ya kujiunga.

Pamekuwa na madai ya Naibu wa Rais kupanga kuhamia chama hicho baada ya misukosuko kuibuka ndani ya chama tawala cha UDA.

Wandani wa Gachagua akiwemo Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga wamelaumu wandani wa Ruto kwa kuhangaisha Naibu wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here