Chama cha Mudavadi chatishia kumbandua naibu rais William Ruto

0

Baadhi ya wabunge wa chama cha Amani National Congress (ANC) kinachoongozwa na Musalia Mudavadi wamemkashifu naibu rais Wiliam Ruto kwa kile wanasema ni kumkosea heshima rais Uhuru Kenyatta.

Wakizungumza katika makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi, wabunge hao wakiongozwa na Ayub Savula wa Lugari wametishia kuwasilisha mswada wa kumuondoa Ruto wakisema anaenda kinyume na katiba kwa kumtusi rais huku wakimtaka kujiuzulu wadhifa wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here