CAS Wavinya kukagua mradi Likoni

0

Kumetokea kioja mjini Mombasa Jumatano asubuhi wakati mhandisi mmoja kutoka China alijaribu kumzuia katibu mkuu katika wizara Uchukuzi Wavinya Ndeti kukagua mradi wa kivukio cha Likoni unaogharimu Sh1b.

Video inayosambaa mitandaoni inamuonesha Wavinya wakijibizana vikali na muhandisi huyo anayesikika akiwaambia kwamba walifaa kumjulisha mapema kabla ya kufika kufanya ukaguzi huo.

Hata hivyo mtu mmoja anaonekana akimvuruta kwa nguvu mhandisi huyo aliyekuwa ameziba mlango wa kuingia kwenye mradi huo na hivyo kumpa nafasi Wavinya na wanahabari kuingia.

Muhandisi huyo anasema hakuwa amefahamishwa mwanzo kuhusu ukaguzi wowote uliokuwa ufanyike.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here