Bunge la kaunti ya Mombasa lafungwa

0

Bunge la kaunti ya Mombasa limefungwa kwa muda wa majuma mawili baada ya waakilishi wadi watatu kupatikana na virusi vya corona.

Naibu spika wa kaunti hiyo Fadhili Makarani amedhibitisha taarifa hizo na kusema hatua hiyo itatoa fursa kwa MCAs wengine kujitenga kuona iwapo wataonyesha dalili za virusi hivyo hatari huku pia majengo ya bunge hilo yakitazamiwa kupuliziwa dawa za kuua virusi hivyo.

Makarani amesema maafisa wengine wa bunge hilo pia wamepatwa na corona lakini hakutoa idadi kamili.

Bunge la kaunti hiyo limekuwa likizoni na MCAs walitazamiwa kurejea siku ya Jumatatu wiki ijayo.

Hofu imeanza kutanda katika kaunti hiyo kutokana na kuanza tena kuongezeka kwa idadi ya watu waliombukizwa virusi hivyo.

Ni hiyo jana ambapo mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Tononoka Mohammed Khamis alifariki baada ya kukutwa na virusi hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here