Bobi Wine ashikwa

0

Mgombea wa urais wa upinzani nchini Uganda Robert Kyangulanyi kwa jina maarufu Bobi Wine ameshikwa na jeshi la Polisi muda mfupi baada ya kuwasilisha stakabadhi zake za kuteuliwa kwa tume ya uchaguzi nchini humo.

Bobi Wine analenga kupambana na rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.

Akizungumza baada ya kupeana stakabadhi zake, Bobi Wine amewaambia wafuasi wake katika ujumbe wa Twitter kuwa sasa “wanaingia katika kipindi muhimu cha kutafuta ukombozi wao”.

Hadi kufikia sasa, wagombea 10 wanawania nafasi ya Urais. Wengine ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Jeshi Jenerali Mugisha Muntu aliyekuwa Waziri wa Usalama Henry Tumukunde.

Mgombea mmoja Patrick Amuriat amekamatwa katika makao makuu ya chama chake cha Democratic Change (FDC).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here