Bintiye Ramadhan Kajembe afariki

0

Familia ya aliyekuwa mbunge wa Changamwe marehemu Ramadhan Kajembe inaomboleza baada ya bintiye mwendazake kufariki.

Langoni Kajembe ameaga dunia akipokea matibabu katika hospitali ya Pandya alipokuwa anapokea matibabu baada ya kupatwa na virusi vya corona.

Ni majuma mawili pekee yalitopita ambapo familia hiyo ilimzika mkewe mwendazake, wote wakifariki kutokana na virusi vya corona.

Inaripotiwa kuwa watu kadhaa wa familia hiyo walilazimika kujitenga baada yao kupatikana na virusi hivyo.

Mwendazake anatazamiwa kuzikwa hii leo kwa mujibu wa dini ya Kiislamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here