BENKI ZARUDISHA SHILINGI MILLIONI 385 KATI YA ZILE ZILIZOPORWA NYS.

0

ASASI za kupambana na ufisadi nchini zimeafikia uamuzi wa nje ya mahakama na benki tano nchini kurejesha pesa zilizofujwa katika sakata ya pili katika shirika la kitaifa la vijana NYS.
Benki za Standard Chartered Kenya, Equity, Diamond Trust, Co-operative, na Kenya Commercial kwa pamoja zimerudisha shilingi million mia tatu themanini na tano, kati ya shilingi billion kumi na moja zilizopotea.
Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji anasema wamelazimika kuafikia uamuzi huo kwani benki hizo na mameneja wake wakuu hawakuhusika moja kwa moja kwenye sakata hiyo.
Mwaka uliopita, benki hizo tano zililazimika kulipa faini ya shilingi million mia mbili sabini na moja baada ya kupatikana na hatia ya kutofuata sheria, hatua iliyochangia kupotea kwa pesa za umma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here