BENKI KUU YAFANYA MABADILIKO KWA NOTI ZA KENYA

0

Benki Kuu ya Kenya (CBK) imefanya mabadiliko manne katika noti zote Kenya.

Mabadiliko hayo ni pamoja na saini ya Gavana wa CBK Kamau Thugge na Katibu katika wizara ya Hazina ya Kitaifa Chris Kiptoo.

Mabadiliko mengine ni pamoja na mwaka wa kuchapishwa kwa noti kuwa 2024, na nyuzi mpya za usalama zenye athari za kubadilisha rangi ambazo ni mahususi kwa kila noti.

Mageuzi hayo yalianza kutekelezwa mwezi agosti ikianza na noti ya shilingi elfu moja na kwa sasa ikiwa ni kwa zile za Sh50, Sh100 Sh200 na 500.

“Tungependa kujulisha umma kwamba noti zilizofanyiwa mabadiliko za Sh50, Sh100, Sh200 na Sh500 zimeanza kusambazwa ,” taarifa kutoka CBK imesema.

Sheria ya Kenya inasema kuwa Saini zilizo kwenye sarafu zinapaswa kuwa za Katibu wa hazina ya kitaifa na Gavana wa Benki Kuu (CBK).

Kustaafu kwa Patrick Njoroge na mageuzi katika wizara ya fedha kumeshurutisha mageuzi hayo kwenye sarafu.

Benki kuu hata hivyo imefafanua kuwa mageuzi yaliyoanza kutekelezwa wakati ambapo noti mpya zilipoanza kutumika mwaka wa 2019 zitasalia.

“Pia tungependa kutoa tahadhari kwa umma kwamba noti nyingine zote zinazosambazwa kwa sasa zinasalia kuwa halali na zitaendelea kusambaa pamoja na noti zilizotolewa,” imesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here