Bendera ya Wiper Machakos kupeperushwa na Agnes Kavindu

0

Agnes Kavindu ndiye atapeperusha bendera ya chama cha Wiper katika uchaguzi mdogo wa useneta kaunti ya Machakos.

Akizungumza alipomkabidhi cheti, kiongozi wa chama hicho Kalonzo Musyoka ameelezea imani yake kuwa Wiper itanyakua kiti hicho kilichobakia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa seneta Boniface Kabaka.

Kavindu ambaye ni mke wa zamani wa aliyekuwa seneta wa Machakos Johnstone Muthama aliwania kiti cha mwakilishi wa akina mama katika kaunti hiyo mwaka wa 2017 na kuibuka wa pili.

Wakati uo huo

Mgombezi wa kiti cha useneta katika kaunti ya Machakos kwa tiketi ya chama cha Maendeleo Chap Chap Mutua Katuku ameelezea utayari wake kuingoza kaunti hiyo kama seneta iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mdogo utakaoandaliwa mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Akizungumza katika ofisi za chama hicho mjini Machakos, Katuku ameahidi kuwahudumia wananchi wa kaunti hiyo bila kuwa mfisadi.

Kiti cha useneta Machakos kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliekuwa seneta Bonface Kabaka mwishoni mwa mwaka jana.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here