Bei za mafuta zapanda

0

Mafuta ya Petroli yameongezwa kwa Sh1.48 huku mafuta ya Diseli na mafuta taa yakipanda kwa senti 0.12 na 0.50 mtawalio kwa kila lita kulingana na bei mpya zilizotangazwa na tume ya kawi nchini EPRA.

Jijini Nairobi, petrol itauzwa kwa Sh105.43, Diseli itapatikana kwa Sh94.51 huku mafuta taa yakiuzwa kwa Sh80.78. Mjini Mombasa, Petroli itauzwa kwa Sh103.05, Diseli ikipatikana kwa Sh92.15 huku mafuta taa yakipatikana kwa Sh80.78.

Wakaazi wa Nakuru watanunua lita moja ya Petroli kwa Sh105.15, Diseli kwa Sh94.54 na mafuta taa kwa Sh83.11. Bei ya Petroli mjini Kisumu itakuwa Sh106.06, Diseli kwa Sh95.35 na mafuta taa kwa Sh84.02

Bei hizo mpya zitatumika kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia kesho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here