Utalazimika kugharamika zaidi kupata mafuta kuanzia hii leo baada ya tume ya kawi EPRA kutangaza bei mpya za bidhaa hiyo.
Mafuta taa yameongzwa kwa Sh18 huku mafuta aina ya Petroli yakipanda kwa Sh3.47 na Diseli ikipanda kwa Sh2.76.
Kufuatia hilo, Petroli lita moja jijini Nairobi itauzwa Sh103.95, Diseli itapatikana kwa Sh94.63 huku mafuta taa yakiuzwa kwa Sh83.65 kwa kila lita.
Mjini Mombasa, Petroli itauzwa kwa Sh101.57, Diseli Sh92.26 na mafuta taa kwa Sh81.29. Mjini Kisumu, Petroli itauzwa kwa Sh104.62, Diseli Sh95.49 na mafuta taa Sh84.54.