BARAZA LA MAGAVANA LAPATA MWENYEKITI MPYA

0
Gavana wa kaunti ya Wajir Ahmed Abdullahi.

Gavana wa kaunti ya Wajir Ahmed Abdullahi Jiir ndiye mwenyekiti mpya wa baraza la magavana (CoG)

Abdullahi amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza hilo baada ya magavana kupiga kura siku ya Jumatatu kuwachagua viongozi wapya katika mkutano ambao ulifanyika jijini Nairobi.

Gavana huyo wa muhula wa pili atamridhi mtangulizi wake katika wadhifa huo gavana wa kaunti ya Kirinyaga Ann Waiguru ambaye amekamilisha hatamu yake kwa kuhudumu kwa mihula miwili baada ya kuchaguliwa mwaka wa 2022 kuongoza baraza la magavana.

Awali gavana Abdullahi alikuwa akishikilia wadhifa wa naibu mwenyekiti katika baraza hilo.

Gavana wa Nyeri Mutahi kahiga ambaye pia alikuwa akimezea mate uwenyekiti amechaguliwa kuwa naibu mwenyekiti huku Muthomi Njuki akisalia kuwa mweyekiti wa kamati ya afya katika baraza hilo.

Magavana Johson Sakaja wa Nairobi, Joseph Ole Lenku wa kajiado ni miongoni mwa waliokuwa wakiwania uwenyekiti.

Abdullahi atahudumu kwa muda wa mwaka mmoja ambapo atakuwa na fursa ya kuwania tena muhula wa pili na wa mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here