Babake waziri Faridah Karoney afariki

0

Familia ya waziri wa Ardhi Faridah Karoney inaomboleza kifo cha babake aliyefariki baada ya kugongwa na pikipiki mjini Kabsabet.

Mzee Edward Kiprotich Karoney, 74, aligongwa na boda boda alipokuwa anavuka barabara kuu ya Kapsabet-Eldoret na alikata roho alipokuwa amekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Kapsabet.

Mzee Karoney alikuwa ameliegesha gari lake kwenye kivuli na alikuwa anajaribu kuvuka barabara hiyo alipogongwa na boda boda hiyo kwa ghafla.

Rais Uhuru Kenyatta amewaongoza viongozi wengine kutuma rambi rambi zake kwa familia ya waziri Karoney kufuatia kifo cha babake aliyekuwa mkulima maarufu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here