BABA NA MJOMBA WASAKWA KWA KUMDHALIMU MWANAO

0

Makachero wa idara ya upelelezi (DCI) kaunti ndogo ya Bunyala wanawasaka Edwin Ogolla na Dennis Asabu ambao wanadaiwa kumdhalimu mtoto mmoja kulingana na video ambayo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Maafisa wa kulida maslahi ya watoto wamefamisha polisi kwamba tukio hilo lilifanyika miezi mitatu iliyopita katika eneo la Musoma.

Inaarifiwa wakati wa kisa hicho, Ogolla ambaye ni mjomba wa mtoto huyo alinaswa kwa kamera akimchapa huku babaye akirekodi bila ya wasiwasi.

Mtoto huyo anaripotiwa kuuguza majeraha ambayo yameangaziwa baada yak isa hicho kugundulika.

Polisi wamesema wanawasaka wawili hao kwa udi na uvumba huku wakidaiwa kutorokea taifa Jirani.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here