Baadhi ya hospitali zinawakataa wakenya wanaotafuta matibabu

0

Baadhi ya wakenya wamekuwa wakirudishwa nyumbani wanapoenda kutafuta huduma za matibabu katika baadhi ya hospitali nchini.

Mwenyekiti wa Tume ya utekelezwaji wa haki, Ombudsman, Florence Kajuju anasema baadhi ya wakenya wamepiga ripoti kwao kuwa wapendwa wao wamefariki baada ya kukataliwa hospitalini.

Elimu

Kajuju pia anaituhumu wizara ya Elimu kwa kukosa kutoa taarifa kamili kuhsuu hatma ya masomo nchini baada ya shule kufungwa hadi Januari.

Kajuju anasema licha ya waziri wa Elimu George Magoha kutangaza kuwa kutakuwa na masomo ya jamii kutumia nyumba kumi, wazazi na wanafunzi hawana taarifa kamili kuhusiana na jinsi hilo litatekelezwa.

Matumizi mabaya ya pesa za umma

Tume hiyo pia imeitaka serikali kuweka wazi matumizi ya pesa zilizotengwa kupambana na janga la corona, na kusema kuwa ni haki ya kila mkenya kufahamu jinsi fedha hizo zilitumika.

Tume hiyo aidha inasema shughuli za huduma kwa umma zimeathirika kwa kiwnago kikubwa tangu virusi vya corona kuripotiwa nchini huku baadhi ya assai muhimu zikitumiwa janga hilo kuwa kisingizo cha kutoa huduma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here