AU yataka Tanzania kuandaa uchaguzi huru na wazi

0

Muungano wa Afrika (AU) umetoa wito wa kuandaliwa kwa uchaguzi huru na wa haki katika taifa jirani la Tanzania hapo kesho.

Mwenyekiti wa AU Moussa Faki amewataka wadau wote wakiwemo wanasiasa kuelekea debeni kwa njia ya amani na kujiepusha na matukio yoyote ambayo yanatatiza amani.

Asasi za kiusalama aidha zimetakiwa kuhakikisha kuwa zimetoa mazingira yatayowawezesha raia wa Tanzania kushiriki katika zoezi hilo kwa njia ya amani.

Haya yanajiri huku upinzani nchini humo ukidai kuwa hadi kufikia sasa watu watano wameuawa katika vurugu huku wengine wakijeruhiwa baada ya polisi kutumia risasi kutawanya raia waliokuwa wamekusanyika.

Hata hivyo jeshi la Polisi limekanusha taarifa hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here