Atwoli na Mutua wamshambulia Kibwana kuhusu kesi ya BBI

0

Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi (COTU) Francis Atwoli amemkashifu Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana akisema hatua yake ya kuelekea mahakamani kupinga mchakato wa BBI ni mbinu ya kuchelewesha marekebisho ya katiba.

Akizungmza huko Kisumu, Atwoli amesisitizia kuwepo kwa haja ya kuharakisha mchakato unaoendelea wa kufanyia katiba marekebisho jambo analosema ni la manufaa kwa taifa hili.

Naye Gavana wa Machakos Alfred Mutua anasema viongozi waliolekeea mahakamani kupinga mchakato wa kufanyia katiba marekebisho kupitia kwa ripoti ya BBI wameogopa kushindwa.

Kiongozi huyo wa chama cha Maendeleo Chap Chap amesema Wakenya wanafaa kuachiwa nafasi ya kufanya uamuzi kuhusu ripoti hiyo wakati wa kura ya maamuzi.

Mutua amesema ripoti hiyo ina manufaa mengi kwa wakenya ikiwemo kuleta pesa karibu na mwananchi na kuwataka wakenya kuiunga mkono.

Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana ameelekea katika mahakama ya kupinga mchakato huo akidai kuwa haujazingatia sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here