ATI ATI YA POLISI WA KENYA NCHINI HAITI UFADHILI WA MAREKANI UKIKATIZWA

0

Taifa la marekani limekatiza ufadhili kwa mpango wa kudumisha usalama nchini Haiti unaoongozwa na maafisa wa polisi wa humu nchini.

Stephane Dujarric ambaye ni Msemaji wa Katibu mkuu wa umoja wa mataifa (UN) Antonio Guterres amesema kuwa wamearifiwa na Marekani kuwa haitatuma mchango wake wa zaidi ya shilingi bilioni 1.7 ($13.3 milioni) kwa kapu la pamoja la kufadhili misheni hiyo.

“Tulipokea taarifa rasmi kutoka kwa Marekani ikiomba kusitisha kazi mara moja kuhusu mchango wao” Amesema Durajiic.

Kusitishwa kwa ufadhili kutoka Washington kunakuja kama sehemu ya msukumo wa Rais Donald Trump wa kupunguza misaada ya Marekani nje ya nchi, harakati ambayo imejumuisha jitihada za kuzima shughuli za shirika kuu la misaada la serikali, USAID.

Zaidi ya watu 5,626 waliuawa nchini Haiti mwaka jana kutokana na ghasia za magenge, takriban elfu moja zaidi ya mwaka 2023, Umoja wa Mataifa ulisema.

Marekani tayari imesambaza dola milioni 15 mchango wa pili kwa ukubwa, baada ya dola milioni 63 zilizoahidiwa na Kanada.

Haiti kwa sasa haina rais wala bunge na inatawaliwa na baraza la mpito, ambalo linapitia changamoto kudhibiti unyanyasaji uliokithiri unaohusishwa na magenge ya uhalifu, umaskini na changamoto nyinginezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here