Askofu wa PCEA Kariuki Kania apewa buriani

0

Askofu wa kanisa la PCEA Peter Kariuki Kania aliyefariki Jumapili iliyopita amezikwa nyumbani kwake Thogoto, kaunti ya Kiambu.

Marehemu ambaye pia alikuwa katibu mkuu wa kanisa hilo la PCEA alifariki akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi baada ya kuonesha dalili za ugonjwa wa Corona.

Naibu rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo chini ya masharti ya wizara ya afya kuwazika watu waliofariki kutokana na COVID19.

Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga walimuomboleza mwenda zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here