Asilimia 80% ya Wakenya wapoteza ajira yasema FKE

0

Asilimia themanini (80%) ya nafasi za kazi zilizobuniwa tangia mwaka wa 2015 katika sekta ya kibinafsi nchini zimepotea kutokana na janga la kimataifa la COVID 19.

 Haya ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirikisho la waajiri nchini FKE na ambao pia unaonyesha kuwa asilimia hamsini ya kampuni zinapanga kupunguza wafanyikazi katika muda wa miezi sita ijayo.

Kulingana na utafiti huo gharama ya kuwalipa wafanyikazi imekuwa ghali mno kwa kampuni nyingi na hivyo kulazimika kupungua wafanyikazi huku ikikadiriwa wafanyikazi milioni moja katika sekta ya kibinafsi watapoteza ajira katika kipindi cha hadi mwisho wa mwaka huu.

Aidha mkurugenzi mkuu wa shirikisho hilo Jacqueline Mugo anataka kampuni kupunguziwa ushuru pamoja na kubuniwa kwa hazina ya mwajiri ili kuwezesha kampuni nyingi kujikimu.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here