Anne Kananu ndiye naibu gavana wa Nairobi

0

Anne Kananu Mwenda ameapishwa rasmi kuwa naibu gavana wa kaunti ya Nairobi dakika chache baada ya kuidhinishwa na bunge la kaunti ya Nairobi.

Kananu amekula kiapo Ijumaa muda mfupi kabla ya saa nane mchana inavyohitajika kisheria katika jumba la mikutano la KICC.

Akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa, Kananu ameahidi kufanya kazi na shirika la NMS sawa na bunge la kaunti ya Nairobi kuwahudunia wakaazi wa jiji.

Bunge la kaunti ya Nairobi lilimuidhinisha Kananu kwenye kikao maalum kilichofanyika hii leo baada yake kupigwa msasa na kamati maalum ikiongozwa na kiongozi wa wengi Abdi Guyo.

Wawakilishi wadi walimtaja Kananu kuwa mchapa kazi na kuonyesha imani yao kuwa ataweza kuongoza kaunti ya Nairobi kufuatia kutimuliwa kwa Mike Sonko.

Kananu ambaye kwa sasa ni afisa wa majanga katika kaunti ya Nairobi aliteuliwa Januari mwaka uliopita lakini mkaaji mmoja akaelekea mahakamnai kupinga uteuzi wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here