Wanajeshi wa kuleta amani nchini Somalia kutoka muungano wa bara Afrika AMISOM wameukombea mji muhimu zaidi kwa mara ya kwanza tangia mwaka huu ulipoanza.
Majeshi hayo yametangaza kuukomboa mji wa Jannale unaotajwa kuwa ngome kuu ya magaidi wa kundi la Alsha baab Machi 17.
Kamanda wa vikosi hiyo Jenerali Tigabu Yilma Wondimhunegn amesema oparesheni hiyo kusini mashariki kwa eneo la Shabelle ilihusisha jeshi la AMISOM pamoja na jeshi la Somalia SNA.
Wanamgambo kadhaa wa Alsha baab waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati wa oparesheni hiyo.
Mji huo wa Jannel alioko kilomo tisini Kusini Magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu umekuwa kitovu cha shughuli nyingi za kigaidi.