AMADI, NYACHAE, WAJUMISHWA KWENYE ORODHA YA WANAOMEZEA MATE UWENYEKITI WA IEBC

0

Kamati ya Uteuzi wa mwenyekiti na makamishna wapya wa Tume ya Uchaguzi na Uratibu wa mipaka IEBC imetoa orodha ya watu waliotuma maombi kujiunga na tume hiyo.

Aliyekuwa msajili wa Idara ya Mahakama Anne Amadi Atieno , aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya utekelezwaji wa katiba ya kenya Charles Nyachae wameorodheshwa miongoni ma wanaomezea uwenyekiti wa tume ya IEBC.

Aliyekuwa mkuu wa Idara ya sheria katika chuo kikuu cha Africa Nazarene ambaye sawia ni mchanganuzi wa maswala ya kisiasa Dancun Ojwang’ ni miongoni mwa watu 37 wanaomezea mate nafasi iliyowachwa wazi baaada ya kustaafu kwa Wafula Chebukati.

Kamati ya Uteuzi ikiongozwa na Nelson Makanda inatarajiwa kuwapiga msasa waliotuma maombi kabla ya kuandaa mahojiano na kuteuwa mwenyekiti na makamishna wapya.

“Tunaowatafuta ni watu walio na uadilifu, uwezo, ujasiri wakutumikia wakenya kwenye tume ya uchaguzi” alisema Makanda.

Makamishna watatu wakiongozwa na Juliana Cherera waliotofautiana na Mwenyekiti wao Chebukati kuhusu matokeo ya Urais walijiuzulu baada ya kuapishwa kwa Rais William Ruto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here