Aliyeua watu 51 New Zealand kukaa jela hadi akufe

0

Mahakama ya New Zealand imempa hukumu ya kifo bila msamaha jamaa aliyepatikana na hatia ya kuua watu 51 kwenye shambulizi la kigaidi.

Brenton Tarrant, 29, raia wa Australia alikubali makosa ya kuwaua watu 51 na kujaribu kuwaua wengine 40.

Akitoa hukumu hiyo, jaji wa mahakama hiyo alitaja kitendo cha mshukiwa  kama kisichokuwa na utu na kwamba hakuonesha msamaha wowote.

Shambulizi hilo lilitekelezwa mwezi Machi na kuishangaza dunia.

Hii ni mara kwanza katika historia ya New Zealand kwa mahakama kutoa hukumu kama hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here