Aisha Jumwa taabani kwa ufisadi

0

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa yuko mashakani baada ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Hajji kuidhinisha kushtakiwa kwake kuhusiana na madai ya ubadhirifu wa Sh57M pesa za ustawishaji maeneo bunge CDF.

Hajji katika taarifa anasema mbunge huyo pamoja na watu wengine saba walitumia ulaghai kupokea pesa kutoka kwa hazina ya CDF pesa ambazo alifaidika nazo moja kwa moja.

Mashtaka yanayomkabili Jumwa pamoja na wenzake ni pamoja na kushirikiana kutekeleza ufisadi, kunyakua mali ya wizi, ulaghai, ulanguzi wa pesa miongoni mwa mengine.

Washukiwa wenza ni Wachu Abdalla ambaye ni meneja wa hazina ya CDF, Malindi, wanachama wa kamati ya kutoa zabuni Kennedy Onyango, Benard Kai, Sophia Charo na Margaret Kalume.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here