Aisha Jumwa kushtakiwa kwa mauaji

0

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji amependekeza mbunge wa Malindi Aisha Jumwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Hii ni kufuatia mauaji ya mwanaume mmoja wakati wa vurugu zilizoshuhudiwa katika wadi ya Ganda kaunti ya KIlifi wakati wa uchaguzi mdogo.

Inaripotiwa kuwa vurugu hizo zilitokea wakati Jumwa na wafuasi wake walivamia mkutano uliokuwa unaongozwa na wapinzani wao kutoka chama cha ODM mkesha wa kuamkia siku ya uchaguzi huo mdogo.

Reuben Katana wa ODM aliibuka mshindi kwenye uchaguzi huo mdogo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here