Aisha Jumwa akana kuiba pesa za CDF

0

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi million tano au shilingi million mbili pesa taslimu baada yake kukanusha kuiba shilingi million 57.

Akitoa agizo hilo, hakimu mkuu wa Mahakama ya Mombasa Edna Nyaloti amesema Jumwa hawezi kukwepa mkono wa sheria wala kutoroka humu nchini ikizingatiwa hadhi yake ya ubunge.

Hakimu huyo pia amepunguza dhamana aliyowapa washukiwa wenza watano kwenye kesi hiyo kutoka shilingi million kumi hadi shilingi million mbili au shillingi laki tano pesa taslimu.

Washukiwa hao wanadaiwa kushirikiana kuiba pesa hizo kutoka kwa hazina ya maendeleo ya eneo bunge CDF.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here