Agnes Wangui adai Justus Murunga alimnunulia shamba Karen

0

Agnes Wangui, mwanamke anayedai kuwa mpenziwe mbunge wa Matungu Justus Murunga anasema marehemu alikuwa amemnunulia shamba Karen, Nairobi na alikuwa anapanga kumjengea nyumba.

Kwenye majibu yake mahakamani, Wangui anasema wamechumbiana kwa muda wa miaka saba matokeo yake yakiwa ni watoto wawili mvulana na msichana.

Kwa muibu wa mwanamke huyo, Murunga alikuwa ameahidi kumuoa kupitia sherehe za kitamadani halafu waanze kuishi Karen kama mtu na mkewe.

Wangui amefaulu kupata agizo la mahakama kusitisha mazishi ya mwendazake ila mjane wa marehemu Christable Murunga amewasilisha kesi ya dharura mahakamani akitaka uamuzi huo kubatilishwa.

Kesi hiyo imeratibiwa kusikilizwa Alhamisi Novemba 26.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here