Wakenya wanahimizwa kuzingatia kwa umakinifu maelezo yanayotolewa na wizara ya afya kuhusu COVID19.
Wito huu umetolewa na rais Uhuru Kenyatta ambaye ameonya kuwa yeyote atakayedhubutu kuhatarisha maisha ya Wakenya kwa kukataa kusalia kwenye karantini atakabiliwa vilivyo kisheria.
Akizungumza mapema Jumatatu asubuhi katika vituo vyetu vya Truth FM na Biblia Husema Broadcasting, msemaji wa serikali kanali smtaafu Cyrus Oguna alisema serikali inafanya kila iwezalo kuzuia kuenea kwa virusi hivyo hatari baada ya watu 15 kudhibitishwa kuambukizwa.
Miongoni mwa tahadhari ambayo Wakenya wametakiwa kuzingatia ni kuosha mikono kila mara na kuepuka maeneo kuliko na mikusanyiko ya watu.