TUME huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC sasa inasema haina ufahamu kuwa Polycarp Igathe alijiuzulu kama naibu Gavana katika kaunti ya Nairobi.
Katika barua kwa spika wa bunge la kaunti Beatrice Elachi, tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Wafula Chebukati inasema haijawahi kupokea barua rasmi kuwafahamisha kuwa Igathe alijiuzulu.
Kupitia kwa wakili wake John Diro, tume hiyo imesema Gavana Mike Sonko alizuiwa kuteua naibu wake kutokana na kesi ya ufisadi inayomkabili.
Haya yanajiri baada ya serikali ya kitaifa kuchukua baadhi ya huduma muhimu ambazo zimekuwa zikitekelezwa na serikali ya kaunti.