Afisa wa Polisi auawa Garissa

0

Afisa mmoja wa polisi ameuawa na mwingine kujehuriwa baada ya  washukiwa wa kundi la kigaidi la Al Shabaab kushambulia kambi ya polisi ya Amuma huko Fafi, kaunti ya Garissa.

Akidhibitisha taarifa hizo, kamanda wa polisi katika eneo hilo Emmanuel Opuru  amesema afisa aliyejeruhiwa anaendelea kupokea matibabu na kutoa hakikisho kuwa afisa huyo yuko hali shwari.

Maharamia hao pia wanaripotiwa kuharibu sehemu ya kuweka silaha katika kambi hiyo na msako wa kuwanasa umeanzishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here