Acheni kumtukana Uhuru, Ruto awaambia wendani

0

Viongozi nchini wametakiwa kuacha kuwatusi na kutumia lugha chafu dhidi ya wenzao.

Akirejelea matamshi ya mbunge wa Emurua Dikkir Johanna Ng’eno na mwenzake wa Kapseret Oscar Sudi, naibu rais William Ruto amesema matusi dhidi ya wazazi wa viongozi wengine au lugha chafu dhidi ya rais Uhuru Kenyatta hayatakubalika.

Badala yake naibu rais kwa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter amewataka viongozi kutumia njia zinazofaa kuelezea hisia zao na wala sio kutumia maneno yenye matusi.

Kulikuwa na hali ya vuta nikuvute Narok wakati Polisi walimshika mbunge Ng’eno kufuatia matamshi yake yaliyolenga kumdhalalisha rais Kenyatta na familia yake na kisha baadaye kutetewa na Sudi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here