Gavana Wamatangi atiwa mbaroni na maafisa wa EACC

0

Maafisa wa upelelezi kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) Jumatano waliripotiwa kumkamata Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi kuhusiana na madai ya ufisadi.

Maafisa wengine tisa wakuu wa kaunti ya Kiambu pia walikamatwa katika msako ambao EACC imesema unahusishwa na uchunguzi wa ufujaji wa fedha za umma na mgongano wa kimaslahi katika mikataba ya ununuzi.

Wapelelezi hao pia walichukua stakabadhi kadhaa na vifaa vya kielektroniki vinavyoaminika kuwa muhimu kwa uchunguzi huo.

Mkurugenzi mtendaji wa EACC Abdi Mohamud anatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusiana na kukamatwa kwa watu hao.

Wamatangi ni Gavana wa pili kukamatwa baada ya uchaguzi mkuu wa 2022 wa kwanza akiwa ni Hillary Barchok wa Bomet aliyetiwa mbaroni mapema mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here