780 waambukiwa corona, 552 wapona, 10 wakufa

0

Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini imefikia 80,102 baada ya watu 780 kupatikana na ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 6,158 katika muda wa saa Ishirini na nne zililzopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa anasema watu wengine 552 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 53,526.

Aidha,wagonjwa 10 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 1,427.

Nairobi imeandikisha visa 273, Kiambu 93, Mombasa 86, Busia 85, Nakuru 40, Turkana 32 na Uasin Gishu 20.

Wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali ni 1,232, 7,295 wanashughulikiwa nyumbani, 57 wako katika chumba cha watu mahututi. Wanaosaidiwa na mashine kupumua ni 32.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here