“TAMBUENI MIILI YA WAPENDWA WENU KABLA HATUJAYATUPA” KAUNTI YA NAIROBI YAHIMIZA

0
city-morturary
city-morturary

Kaunti ya Nairobi imetoa wito kwa umma kutambua miili ya watu 107 ambayo haijadaiwa na wapendwa wao katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City.

Katika taarifa kutoka kwa Idara ya Afya, Ustawi na Lishe Kaunti hio imewataka wale ambao wamepoteza mawasiliano na wapendwa wao au hawana uhakika waliko kuzuru Mochwari ya City na kuthibitisha ikiwa jamaa zao ni miongoni mwa waliohifadhiwa humo.

Kaunti hiyo imesema kwa sasa, Chumba cha kuhifadhi Maiti kina miili iliyozidisha uwezo wake na kina nuia kusaka agizo la mahakama kutupa miili ambayo haijadaiwa.

“Umma unahimizwa kusaidia kwa kuwatambua wapendwa wao, ili kupunguza shinikizo linalokumba wafiwa,” Kaunti imesema.

Ikinukuu Sheria ya Afya ya Umma sura ya 242, Kaunti imesema kwamba miili lazima ihifadhiwe kwa angalau miezi mitatu kabla ya ruhusa ya korti kupatikana ili kutupwa.

“Kufuatia kipindi hiki, notisi kwa umma ya siku 14 inahitajika kabla ya hatua zozote zaidi kuchukuliwa,” Kaunti imeongeza.

Septemba mwaka huu kaunti hio ilinyimwa agizo la kutupa miili; mahakama ikiagiza mwanasheia mkuu kutoa maelezo kuhusu uwezekano wa ongezeko la miili kuwa ilitokana na mauaji ya waandamanaji waliokuwa wakipinga serikali.

Hivi sasa, Chumba hicho kina zaidi ya miili 600, ilhali uwezo wake ni 184 tu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here