Shirika la Transparency International (TI) limeelezea wasiwasi wake kuhusu matumizi ya pesa zilizotengwa kwa minajili ya kukabiliana na janga la corona.
TI kupitia taarifa inasema maswali yaliyoulizwa na bunge kuhusu zilivyotumika Sh1.3b bado hayajapata majibu huku Wakenya wakisalia gizani kuhusu ni vipi pesa hizo za mlipa ushuru zimetumika.
Katika mapendekezo yake, shirika hilo linaitaka serikali kuweka wazi maelezo kuhusu zilivyotumika pesa hizo kwa kuzingatia uwajibikaji.
TI vile vile imetoa changamoto kwa kila kaunti kuweka wazi pesa zilizotengwa hususan kukabiliana na janga hilo na iwapo lengo hilo limeafikiwa.