SAFARI YAKATIZWA ABIRIA WAKISHAMBULIWA MOYALE

0
Shambulizi Moyale
Shambulizi Moyale

Watu wasita wamedhibitishwa kujeruhiwa kufuatia kushambuliwa kwa basi walimokuwa wakisafiria kati ya  eneo la Bori na Dadach Lakole katika kaunti ndogo ya Moyale jana usiku.

Kulingana na polisi, basi hilo lililokuwa likitoka Moyale kuelekea Nairkobi na abiria 50, lilishambuliwa na watu wasiojulikana na waliojihami kwa bunduki na kuanza kumimunia basi hilo risasi.

Inaarifiwa sita hao wanapokea matibabu katika hospitali ya kimisheni ya Sololo huku mmoja akiwa kwenye hali mahututi na mtu mmoja akifahamika kuaga dunia.

Ripoti zinaashiria muda mchache baada ya kisa hicho cha saa nne usiku, gari aina la Toyota Land Cruiser pia lilishambuliwa na watu waliojihami kwa bunduki.

Mtu mmoja kati ya waliokuwa ndani ya gari hilo alipigwa risasi na kuaga dunia huku dereva akitoroka bila ya majeraha yoyote.

Kisa hiki kinajiri wiki chache baada ya kingine kama hicho eneo la Elle Bor/Forolle ambapo watu wasabi waliuwawa na lori kuchomwa na watu wanaodaiwa kutoka Ethiopia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here