Idadi ya visa vya ugonjwa wa corona nchini inakaribia kufika 20, 000 baada ya watu 788 kupatikana na ugonjwa huo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema hii inafikisha 19,913 jumla ya visa vya ugonjwa huo kufikia sasa.
Waliofariki kutokana na ugonjwa huo wamefikia 325 baada ya kukufa kwa watu wengine 14 huku waliopona wakifikia 8,121 baada ya kupona kwa watu 100.
Nairobi imerekodi visa 487, Kiambu 86, Nakuru 34, Kajiado 26, Mombasa 25, Machakos 21, Busia 20, Narok 14, Bomet 9, Kericho 8, Siaya na Kisumu 8, Uasin Gishu, Baringo na Nyeri 5.
Katika jiji la Nairobi, Langata inaongoza kwa kuripoti visa 58, Westlands 50, Dagoreti North 42, Embakasi East 39, Makadara 34, Embakasi South & Starehe 32, Embakasi West 30, Roysambu 29, Kasarani 28, Ruaraka & Kibra 19, Dagoreti South 19, Embakasi North 18, Embakasi Central 14 & Mathare 10.