Askofu mwenye Utata Gilbert Juma Deya asubuhi hii amepata afueni baada ya mashtaka dhidi yake ya kuiba watoto watano kufutiliwa mbali

Hakimu mkuu mwandamizi wa Milimani Robison Ondieki aliamua kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuwasilisha kesi dhabiti dhidi ya Deya.

Hakimu Ondieki amesema kuwa upande wa mashtaka ulikosa kudhibitisha kuwa Deya alikuwa sehemu ambapo watoto hao walipopatikana au kuonyesha kwa njia yoyote kuwa Deya alihusika na wizi huo.

Mahakama hio imesema kuwa wakati ambapo watoto hao walikuwa wakiibiwa Deya alikuwa katika Taifa la Uingereza.

Hakimu huyo alisema licha ya mkewe Mary Juma kushtakiwa kwa kosa kama hilo, pia aliachiliwa na mahakama ya Kibera.

Deya alipata umaarifu katika miaka za nyuma kwa kudai kuwa anauwezo wa kuwasaidia Wanawake tasa kupata watoto na kuhusishwa na sakata ya ulanguzi wa watoto ulikuja kutambulika kama ‘Miracle babies.’