RUTO WITH ALL CAS's

Mahakama imehairisha kutolewa kwa uamuzi wa kesi ya kupinga kuteuliwa kwa makatibu waandamazi wa serikali ya kenya kwanza.

Kesi hio iliratibiwa kuamuliwa saa tatu asubuhi ila imesongezwa hadi alasiri ya leo majaji wakitarajiwa kuwasilisha uamuzi wao saa nane mchana.

Majaji Alnir Visram, Hedwig Ongundi na Kanyi Kimondo watatakiwa kuamua iwapo Rais William ruto alikiuka sharia kwa kuteua makatibu waandamizi 50 badala ya 23 waliopendekezwa na tume ya Huduma ya Umaa.

“Kifungu cha 3 cha Katiba kinaamuru wahusika wote kukataa uteuzi wowote usio wa kikatiba, afisi, au kufaidika kama jukumu lao la kibinafsi la kutetea na kulinda katiba,” walalamishi walisisitiza.

Rais Ruto alitetea uamuzi wake wa kuteua CAS 50 kuwa manaibu wa Mawaziri 22 akitaja kuwa wanamajukumu mengi katika serikali yake.

Rais Ruto alieleza kuwa ili atekeleze manifesto ya Kenya Kwanza Alliance, alihitaji maafisa zaidi.

“Katika kuteua CAS huo ndio mpango wa serikali yangu. Ni uamuzi wangu na naona haja ya CAS kuwa pale katika serikali yangu,” Ruto alisema.

Baadhi ya walioteuliwa kama Makatibu Waandamizi ni pamoja na Mwanablogi Denis Itumbi(Wizara ya Teknolojia), Millicent Omanga(Usalama wa Ndani), Evans Kidero (Uchuuzi), Charles Jaguar (Michezo) miongoni mwa wengine

Kesi hio iliwasilishwa na Chama cha mawakili humu nchini na Mkenya anayeishi Ugahaibuni Karanja Matindi.