Muungano wa Azimio la umoja hii leo inatarajiwa kuandaa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kamkunji jijini Nairobi ambapo unatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu hatua watakazochukua baada ya kupitishwa kwa mswaada wa fedha 2023.
Muungano huo umekashifu serikali ya Kenya Kwanza kwa kile umetaja kama kupuuza matakwa ya wakenya na kupitisha mswaada wa fedha licha ya lalama kutoka kwa wananchi.
“Utawala wa Rais Ruto umehakikisha kuwa mapenzi ya wakenya yamepuuziliwaa. Badala yake umedumisha ushuru dhalimu kwa bidhaa za petrol, majumba na ushuru.” Alisema Kinara mwenza wa muungano huo Martha Karua katika kikao na wanahabari.
Azimio imesema kuwa mkutano wa leo utawapa wakenya ambao sauti yao haikusikika bungeni nafasi ya kuwasilisha pingamizi dhidi ya uamuzi wa Bunge kupitisha mswaada wa fedha.
Karua aidha amesema kuwa wakenya wanapswa kukaza mkanda kwani gharama ya maisha itapanda baada ya bajei kupitishwa.
“Ingawa kumekuwa na Mfumuko wa bei za bidhaa ni lazima sasa mwannchi ajitayarishe kupanda hata Zaidi kwa bidhaa msingi. Kile kidogo tulichobaki nacho lazima kitayeyuka” Alisema Karua.
Kinara wa Upinzani Raila Odinga anatarajiwa kutuwa katika uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kbala ya kuelekea Kamkunji kuongoza mkutano wa leo.
Akihojiwa na kituo kimoja cha Kifaransa Rais William Ruto alisema kuwa utawala wake hautatibua mikutano na maandamano ya Azimio iwapo yatakuwa ya amani.
“Sina tatizo na Odinga. SIna tatizo na maandamano. Kile nimesihihi upinzani ki kuwa wasijihusishe na vurugu na uharibifu wa mali. Sisi ni demokrasia.” Rais aliambia kituo cha France 24.