BUNGEI

Maafisa wa Polisi wamesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja uko huru kufanya mkutano wao wa mashauriano jijini Nairobi.

Mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei umesema muungano huo ulikuwa umewaarifu kuhusu mkutano uliopangwa kufanyika katika uwanja wa Kamkunji eneo la Muthurwa.

Bungei amesema polisi wamejipanga kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa amani pasi na vurugu.

“Tuko tayari kuhakikisha mkutano huo unakuwa wa amani. Tutatoa usalama unaohitajika,” alisema Bungei.

Makumi ya maafisa wa polisi wameonekana kwenye mitaa ya jiji la Nairobi na kwenye uwanja wa Kamkunji

Tangazo hilo la polisi linakuja kabla ya mkutano uliopangwa kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa Azimio na wafuasi wao kupinga Mswaada wa Fedha, 2023.

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga anatarajiwa kurejea nchini asubuhi ya leo baada ya mapumziko marefu nchini Poland.