CAS Itumbi akiwa mahakamani

*Mahakama ya Milimani imeridhia ombi la Mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) la kumwondolea kesi inayomkabili katibu mwandamizi katika wizara ya teknolojia Dennis Itumbi.

Itumbi alikuwa amefunguiwa mashtaka ya kuhusishwa na barua tata Iliyoeleza njama ya kumuua rais Wiliam Ruto mwaka wa 2019 wakati huo akiwa Naibu wa Rais.

Katika uamuzi wake Hakimu wa mahakama ya Milimani Susan Shitubi ametupilia mbali kesi hio akihoji kuwa ni kinyume na sheria.

“Na sikitikia kuwaondolea mashtaka washtakiwa ila katiba inaniruhusu kusitisha kesi iwapo mshatakiwa anadaiwa kukiuka kipengee cha sheria anbayo haiambatani na katiba.” Alisema Hakimu Shitubi.

Kulingana na Mkurugenzi wa mashtaka, hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwafungulia mashtaka Itumbi na mashtakiwa mwenza Samwel Gakeri.

Katika kesi hiyo, Itumbi alikabiliwa na makosa matatu ikiwemo kuandika waraka wa uongo, kuchapisha taarifa ya uongo, na kuhusisha simu yake ya mkononi, madai ambayo alikanusha.

Itumbi anadaiwa kuchapisha barua iliyodai kuwa baadhi ya mawaziri waliandaa mkutano katika hoteli ya Lamada kupanga kumuua Rais Ruto.