Mtangazaji tajika wa Injili James Mahmi amejiunga na Kituo Cha Truth FM. 

Mahmi ambaye kabla ya kujiunga na Kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la AIC Kenya alikua alifanya kazi katika Kituo Cha Pearl Radio sasa atafanya kipindi Cha ‘DawnBreak’ kuanzia saa 11 asubuhi Hadi saa 3 asubuhi.

Mtangazaji na mhudumu huyo ameashiria furaha ya kurudi katika Kituo hicho alichoghura miaka mitatu iliyopita.

“Ni furaha kurejea nyumbani. Umekua muda mrefu. Niko tayari kuburudika na kuhimizana pamoja na wasikilizaji wa Truth FM “alisema Mahmi.

Kabla ya kuondoka alifahamika zaidi kwa kitengo Cha ushuhuda almaarufu “The Big Testimony” iliyowapa wakristo nafasi ya kuelezea matendo ya Mungu maishani mwao.

Mtangazaji mwenza Terry Njuguna kwa upande wake ameashiria furaha kufanya kazi na Mahmi akimtaja kama ‘Rafiki’.

“Ni Mahmi aliyenikaribisha katika ulimwengu wa radio miaka kadhaa iliyopita. Nashukuru kwa kua ntakua na fanya kazi na mtu ambaye naeza muita rafiki” alisema Terry.

Katika mpangilio mpya wa vipindi katika Kituo Truth FM, Njuguna Pamoja na Mahmi watafanya kipindi Cha Dawnbreak.

Mtangazaji wa zamani na mcheza santuri DJ Terots akirejelea kipindi Cha “Gospel Switch” , Stella Gatogo Nanzoi pamoja na Brown Karinga wakifanya kipindi Cha “Truth Express” nae MK akisalia katika kipindi Cha True armor na pia kipindi cha Truth Kids na Teacher Monicah kikirejea hewani kila siku ya Jumamosi saa 2 hadi saa 4.