Rais William Ruto amepinga hatua ya Kinara wa Upinzani Raila Odinga yakuandaa maandamano kupinga kubanduliwa afisini kwa makamishana wanne wa tume ya Uchaguzi IEBC.

Akizungumza katika kampuni ya Usambazaji chakula ya Twiga Rais Ruto ametaka upinzani kudumisha amani wakati wanapoendesha shughuli yao ya kujukumisha serikali.

Ruto ametaka upinzani kutochochea wakenya dhidi ya wenzao akisema kuna njia mbadala ya kupinga serikali wala sio kuelekea barabarani.

“Nataka kuambia ndugu zetu wa upinzani kua tunakubali kujukumishwa lakini hatutaki mugawanyishe na kugonganisha wakenya dhidi ya wenzao” alisema Rais.

Kauli yake inajiri baada ya Odinga kutangaza kua kuanzia juma tano wiki hii ataandaa viakao vya kupata maoni ya umaa kuhusu kuondolewa afisini kwa makamishna Juliana Chereara, Francis Wanderi , Justus Nyangaya na Irene Masit.

Odinga na viongozi wengine wa Azimio wamepinga hatua ya kuondolewa kwa Wanne hao wakisema wanaaandamwa kwa kusimama na ‘ukweli’.

Naibu wa Rais Rigathi Gachagua Siku ya jana alisuta Odinga kwa kile alitaja kama ‘kutumia watoto maskini’  kutimiza malengfo yake ya kibinafsi.

“Tunawambia kama wanataka kuandaa maandamano watumie watoto wao. Haiwezekani wanateua watoto wao kuenda EALA alafu watumie watoto wetu kuandamana. “ Alifoka Gachagua.

Azimio linadai kua Ruto anadhamiria kuwaondoa wanne hao na kuteua makamishna wanaoegemea katika mrengo wake ili kurahisisha ushindi wake katika uchaguzi wa 2027.