Jengo hilo liliporomoka mwendo wa saa kumi asubuhi ya leo baada ya zaidi ya wapangaji 100 kuhamishwa jumapili mchana baada ya nyufa kutoakea kwenye miamba ya ghorofa hilo.

Tayari shughuli za uokozi zimeanzishwa ila haijabainika iwapo kuna mtu yeyote amefunikwa na fusi za jengo hilo ambalo liko karibu na kituo cha polisi cha Ruiru.

Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi aliyeongoza shughuli ya kuhamisha wapangaji jana amesema watakaopatikana na hatia ya ujenzi duni na kukiuka maagizo watachukuliwa hatua.